13 Aprili 2025 - 22:37
Source: Parstoday
Taasisi ya Palestina: Jamii ya kimataifa isaidie sekta ya afya na tiba ya Gaza

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imelaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuishambulia Hospitali ya Al Maamadani na kuitaka jamii ya kimataifa kuisaidia sekta ya afya na tiba ya eneo hilo.

Wizara hiyo imeziomba taasisi za kimataifa na mashirika mengine kuisaidia sekta ya afya na tiba ya Gaza kwa mujibu wa sheria na hati za kimataifa na kibinadamu na kuulazimisha utawala wa Kizayuni usitishe hujuma zake dhidi ya Gaza hasa mashambulizi dhidi ya hospitali na sekta ya afya ya eneo hilo. 

Imeelezwa kuwa, jeshi la Israel limeshambulia kitengo cha kupokea wagonjwa wa dharura na duka la dawa katika Hospitali ya Al Maamadani. Katika mashambulizi hayo na mapema leo, makumi ya wagonjwa wa Kipalestina wamejeruhiwa na kulazimika kuhamishiwa katika mitaa ya kandokando ya hospitali hiyo. 

Ripoti ya al Jazeera imeeleza kuwa, jengo  hilo la hospitali limelengwa kwa makombora mawili na kuharibiwa pakubwa. 

Kuhusiana na hili, Mirjana Spoljaric Egger, Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu amedokeza kwamba sasa tumo katika hali ambayo ningeiita ni Jahanamu ya duniani na kwamba wakazi wa Gaza hawana maji, umeme na chakula. 

Mirjana Spoljaric Egger ameeleza kuwa: Hakuna msaada wowote ulioingia Gaza tangu Israel ilipozuia kuingia kwa malori ya misaada ya kibinadamu katika eneoi hilo mnamo Machi 2. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha